Uzinduzi wa Shule ya Ufundi na Dini ya Markaz Al-Mustafa unachukuliwa kama hatua muhimu katika kuendeleza azma ya taasisi za Kiislamu nchini Tanzania katika kuandaa kizazi cha vijana wanaochanganya ujuzi wa kisasa na maadili ya Kiislamu.
Kwa Mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Hafla Kubwa ya uzinduzi wa Shule ya Ufundi na Dini ya Markaz Al-Mustafa imefanyika kwa mafanikio makubwa Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Shule hii mpya imekusudiwa kuwa kituo cha kielimu kitakachowawezesha vijana kupata elimu ya kiufundi pamoja na elimu ya dini, kwa lengo la kujenga jamii yenye uelewa mpana, maarifa na maadili bora ya Kiislamu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali za Kiislamu, wazazi, wanafunzi, na wananchi wa maeneo jirani. Tukio hilo lilipambwa na ugawaji wa vyeti kwa wahitimu wa shule, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi safari ya kielimu yenye mwelekeo wa kiroho na kimaendeleo.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Samahat Sheikh Salmani Mwagwe, Kiongozi Mkuu wa Taasisi ya Ahlul-Bayt (as) Afrika Mashariki na Kati, ambaye katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa kuunganisha Elimu ya Dunia na Elimu ya Dini. Alisema:
“Uislamu unahimiza elimu ya pande zote - elimu inayomjenga mtu kimaadili na kiufundi. Vijana wetu wanapaswa kuwa mabingwa wa maarifa, wabunifu na wacha Mungu katika jamii zao.”
Kwa upande wake, viongozi wa Markaz Al-Mustafa walitoa shukrani kwa wadau wote waliochangia kufanikisha ujenzi na uanzishaji wa shule hiyo, wakiahidi kuendeleza juhudi za kutoa elimu bora yenye misingi ya uadilifu, ujuzi na heshima kwa dini.
Uzinduzi wa Shule ya Ufundi na Dini ya Markaz Al-Mustafa unachukuliwa kama hatua muhimu katika kuendeleza azma ya taasisi za Kiislamu nchini Tanzania katika kuandaa kizazi cha vijana wanaochanganya ujuzi wa kisasa na maadili ya Kiislamu.
Your Comment